Kimalay cha Sabah

Kimalay ya Sabah ni lugha ya Kiaustronesia nchini Malaysia inayozungumzwa na Wamalay. Mwaka wa 2013 idadi ya wasemaji wa Kimalay ya Sabah imehesabiwa kuwa watu milioni tatu lakini wengi wao hutumia Kimalay ya Sabah kama lugha ya mawasiliano tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimalay ya Sabah iko katika kundi la Kimalayiki. Wengine huiangalia kama lahaja ya Kibrunei.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search